Wednesday, August 8, 2012

5:52 PM
Mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara katika msimu wa 2011/12, John Raphael Bocco ametwa kufanya majaribio Afrika kusini katika klabu ya Super Sport kufuatia kufanya vyema katika michuano ya kombe la Kagame akiwa na uzi wa Azam FC.
Bocco anataraji kwenda Afrika Kusini agust 11 mwaka huu kwa ajili ya majaribio ambapo safari hii itakuwa ni mara ya pili baada ya ile ya awali ya Israel katika klabu ya Tel-Aviv.

"Azam FC imepokea barua ya mwaliko wa majaribio toka klabu ya Super Sport ya Afrika Kusini kwa mchezaji John Bocco ambapo atapaswa kusafiri Jumamosi tarehe 11/08/2012 kwenda Johannesburg Afrika ya Kusini. Jogn Bocco atatumia muda wa wiki moja nchini Afrika ya Kusini. Uongozi wa Azam FC unampongeza John Bocco kwa mafanikio haya na unamtakia kila la heri kwenye majaribio yake," ili eleza taarifa ya Azam FC katika ukurasa wa facebook wa timu hiyo yenye maskani yake Chamanzi.

0 comment.:

Post a Comment