Timu ya kenya inayo julikana kwa jina la leopard fc-football club itawasili kesho wakiwa tayali kupambana na simba sport club na yanga sport club katika uwanja wa taifa jijini dar-es-salaam mechi ya kirafiki kwa ajilli ya kujianda naligi kuu ya tanzania bara Akizungumzia
ujio wa timu hiyo, Mratibu wa mechi
hiyo,
Kennedy Mwaisabula alisema kila kitu
kinakwenda
vizuri na wanatarajia mechi hizo
zitajaa
upinzani mkali kutokana na jinsi timu
hiyo
ilivyo.
"FC
Leopards ni timu nzuri kila mmoja anaijua
kwani
inaupinzani mkali sana katika Ligi Kuu ya
Kenya, na
ndio maana tukaiomba ije kwa ajili ya
kuzinoa
timu zetu," alisema Mwaisabula.
Kwa
upande wake Kocha Mkuu wa Simba Milovan
Cirkovic
alisema mechi hiyo itakuwa kipimo kizuri
kwa
wachezaji wake wapya kwani ataweza kubaini
mapungufu
katika kikosi chake.
"Ni mechi
nzuri ambayo naimani kabisa
itaniwezesha
kujua mapungufu katika kikosi
changu,
hivyo nawataka wachezaji wangu waitumie
vizuri
kwani ninafasi nyingine kwao katika
kutafuta
namba katika kikosi cha kwanza," alisema
Milovan.
Alisema
wakicheza mechi hiyo atatafuta mechi
nyingine
zaidi ili aweze kukipika vizuri kikosi
chake,
kwani katika michuano ya Kombe la Kagame
aligundua
mapungufu mengi.
2:18 PM
0 comment.:
Post a Comment