Saturday, September 8, 2012

11:24 AM
kikosi cha young african
mchezaji wa young african -Tanzania
YangaSportClub leo imefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya4-0 moro united inayo julikana timu nzuri  tanzania, katika mchezo wakirafiki zidi ya Yanga SportClub  uliochezwa katika uwanja  wa Taifa Dar-es-salaam,Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu leo amefungua rasmi akaunti yake ya mabao Yanga, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi huo, mabao mengine yakitiwa kimiani na beki Juma Abdul na kiungo Shamte Ally.kocha wa yanga tom saintfiet raia wa ubelgiji alitaka mechi moja dhidi ya timu inayocheza kama wapinzani wao wa kwanza katika Ligi Kuu, Prisons na pia katika Uwanja mbaya kama ambao atachezea mechi ya kwanza ya ligi hiyo, Sokoine mjini Mbeya na ndiyo maana timu hiyo imecheza mechi hiyo leo kwenye Uwanja huo.
Saintfiet ameridhika na kiwango cha timu na sasa anasema timu iko tayari kwa Ligi Kuu, akianza na Prisons iliyorejea Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Septemba 15.
Hiyo inakuwa mechi ya 11, Saintfiet anashinda Yanga katika mechi 12 tangu ajiunge nayo miezi miwili iliyopita.

0 comment.:

Post a Comment