KLABU ya
Azam imeomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye
Uwanja wake wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex ulioko Chamazi badala ya
Uwanja wa Taifa.
Kuhusu
maombi hayo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema yatawasilishwa kwenye
kikao cha Kamati ya Ligi ya TFF kinachotarajiwa kufanyika leo mjini Dar es
Salaam.
TFF iliamua
mechi zote za Simba na Yanga dhidi ya timu za Dar es Salaam na Pwani, zichezwe
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa sababu ya idadi kubwa ya mashabiki
wanaotarajiwa kuingia uwanjani, wakati viwanja vya Chamazi na Mabatini, Mlandizi
unaotumiwa na Ruvu Shooting ni vidogo.
Awali, TFF
ilipanga Ruvu Shooting na Yanga zicheze kwenye Uwanja wa Chamazi pia Oktoba 20,
mwaka huu, lakini klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),
kitengo cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imeomba mechi hiyo ichezwe Uwanja wa
Taifa.
Ingawa Ruvu
Shooting haijasema sababu za kuomba mechi hiyo ichezwe Taifa badala ya Chamazi,
lakini dhahiri wanataka kunufaika na mapato kutokana na ukubwa wa Uwanja wa
Taifa.
0 comment.:
Post a Comment