JOHN BOCCO,NDIYE ALIYEFUNGA MAGOLI YOTE2-0. |
MSUVA AKIMTOKA MCHEZAJI WA SUDAN. |
MASHABIKI WA TANZANIA WAKIJA KUWAPA SUPPORT TIMU YAO. |
TIMU ya soka
ya taifa ya Tanzania Bara, imeanza vema kampeni zake za kuwania Kombe la Mataifa
ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, baada ya kuichapa mabao
2-0 Sudan katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Mandela,
Namboole, Kampala, Uganda.
Ushindi huo,
unaiweza Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika nafasi ya pili kwenye msimamo
wa Kundi B, nyuma ya Burundi inayoongoza kwa wastani wa
mabao.
Hadi
mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yote yakipachikwa kimiani na
mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyetumia vema krosi za
Mrisho Khalfan Ngassa.
Bocco
alifunga bao la kwanza Bocco aliiwahi vema krosi ya Ngassa aliyewatoka mabeki wa
Sudan wingi ya kushoto na kuitumbukiza kimiani dakika ya
14.
Adebayor wa
Chamazi aliwainua tena vitini mashabiki wa Tanzania dakika ya 28, akiunganisha
krosi ya Ngassa tena kutoka kule kule kushoto.
Kwa ujumla
Tanzania Bara walicheza vizuri kipindi cha kwanza, wakishambulia zaidi kupitia
pembeni, kulia Simon Msuva ambaye hakuwa na madhara sana na kushoto Ngassa
ambaye alikuwa mwiba mchungu haswa kwa Wasudan.
Pamoja na
Bara kutawala kipindi cha kwanza, lakini Wasudan walifanya mashambulizi kadhaa
ya kushitukiza na sifa zimuendee mlinda mlango Juma Kaseja, ambaye alioko
amichomo miwili ya hatari mno.
Kipindi cha
pili Stars, inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen iliendelea kutawala mchezo,
lakini safu ya ulinzi ya Sudan iligangamala.
Tanzania Bara; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomari
Kapombe, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba, John Bocco,
Mwinyi Kazimoto na Simon Msuva/Shaaban Nditi.
Sudan; Ebd Elrahman Ali, Moawia El Amin, Sami Abdallah, Faris
Abdallah, Hamoda Bashir/Farid Mohamed, Mohamed El Mortada, Sadam Abutalib,
Mohamed Mussa Idris, Modathir Mohamed, Adam Sayer/Osama El Rashid na Mohamed
Osman/Saed Siddig.
Katika
mchezo wa awali, Burundi walishinda mabao 5-1, mabao yake yakifungwa na Chris
Nduwarugira dakika ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman
Ndikumana dakika ya 84 na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril kwa
penalti dakika ya 55.
Matokeo hayo
yanalifanya Kundi B lizidi kuwa gumu, kwani Burundi inaongoza kwa pointi zake
tatu na mabao mengi, Tanzania ya pili kwa pointi tatu na mabao mawili- lakini
bado Sudan wanaweza kupata matokeo mazuri katika mechi
zijazo.
NENO LA LEO LANGU
MUNGU BARIKI TANZANIA MUNGU BARIKI WACHEZAJI WAKE.
0 comment.:
Post a Comment