Thursday, February 7, 2013

4:51 PM

Timu ya taifa ya Cameroum wametota katika uwanja wa taifa baada ya kuduwazwa na soka ya timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa stars' na wakiala kwa goli moja bila majibu.Katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa taifa, katika kipindi cha kwanza mchezo ulikuwa sawa na timu zikishambuliana kwa zamu, huku stars wakijaribu kila namna ya kupata goli kwa kutumia mashuti na kushambulia kutoka pembeni.
Katika dakika ya 26 stars walipata mkwaju wa penati baada ya beki wa Cameroun kuunawa mpira katika eneo la hatari na Erasto Nyoni alipoteza penati hiyo na kupelekea timu kwenda mapumziko bila kusguhudia goli lolote.
Katika kipindi cha pilh stars walirejea kwa kasi na kuonyesha kandanda safi na la kuvutia na katika dakika ya 89 Mbwana Ally Samata aliipatia goli la ushindi akiunga pande la Erasto Nyoni.

Kikosi cha stas kilicho anza leo;
JUMA KASEJA
ERASTO NYONI
SHOMARI KAPOMBE
AGGREY MORISE
KELVIN YONDAN
SALUM ABOUBAKARY
MRISHO NGASSA
FRANKY DOMAYO
MBWANA SAMATA
MWINYI KAZIMOTO
AMIR KIEMBA

0 comment.:

Post a Comment