Friday, September 28, 2012

7:19 PM


Azam FC walipata goli la kuongoza katika kipindi cha Kwanza dakika ya 44 kupitia kwa John Bocco 'Adbayor' akifunga goli lake la kwanza msimu huu wa 2012/13 kwa mkwaju wa penati.

Azam FC walirejea kipindi cha pili na kutawala mchezo na kufanikiwa kupata magoli mengine mawili kupitia kwa mapacha Kipre Herman Tcheche dakika ya 65 na Kipre Michael Balou dakika ya 79.

Kwa matokeo hayo Azam FC wamerejea kileleni mwaligi kwa mda wakingoja mchezo wa kesho kati ya Simba SC na Tanzania Prisons ya Mbeya.

0 comment.:

Post a Comment