Brandts wa pili kutoka kulia, akiwa na viongozi wa Yanga. Kulia ni Seif Magari. Kushoto kwake ni Bin Kleb na Majjid |
Anapakia mizigo kwenye gari la Bin Kleb |
Anazungumza na Waandishi wa Habari |
Akiwa na viongozi wa Yanga |
Kulia kwake Bin Klerb, kushoto Mwalusako |
Anatoka Uwanja wa Ndege |
KOCHA mpya
wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, beki wa zamani wa
kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Holanzi, amewasili usiku huu
(saa 3:45) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na
ndege ya KLM tayari kusaini mkataba na kuanza kazi katika klabu
hiyo.
Brandts
amepokewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako na viongozi wengine,
Abdallah Ahmad Bin Kleb, Seif Ahmad ‘Magari’ na Majjid Suleiman na amesema
anaijua Yanga ni timu nzuri, kubwa hana shaka ataiwezesha kufanya vizuri katika
medani ya soka Afrika.
Yanga,
imetimiza malengo yake ya kuwa kocha mpya, kabla ya kucheza na wapinzani wao wa
jadi, Simba SC, Oktoba 3, mwaka huu baada ya kumfukuza Mbelgiji, Tom Saintfiet,
kutokana na kuwasili makubaliano na Brandts, ambaye ataanza kazi mara moja
kesho.
Mholanzi
huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga, baada ya Mbrazil
Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya
pili.
Mtaalamu
huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali na
PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De
Graafschap.
Brandts
aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na pia
alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978.
Katika
fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa
mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za
Kombe la Dunia.
Alianza
kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi
ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi
na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
Alipostaafu
soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa
hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya
tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha
mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa
2008–2009.
Akateuliwa
kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia
APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako ‘riziki’ yake imeisha miezi miwili iliyopita na
sasa amepata maisha mapya Yanga.
Akiwa APR,
Brandts alifungwa mechi zote mbili na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Mbelgiji
Tom Saintfiet katika Kombe la Kagame, moja ya makundi 2-0 na nyingine ya Nusu
Fainali 1-0. Yanga iliibuka bingwa, ikiifunga Azam FC 2-0 kwenye
fainali.
Brandts
atakutana na wachezaji wake wa zamani wawili Yanga, beki Mbuyu Twite anayeanza
msimu wa kwanza katika klabu hiyo na kiungo Haruna Niyonzima anayeingia katika
msimu wa pili, ambao alifanya nao kazi APR.
0 comment.:
Post a Comment