Monday, September 10, 2012

4:23 PM

KOCHA wa Sofapaka ya Kenya, David Ouma,
 amesema angependa kuwasajili wachezaji Mrisho Ngassa na beki Amir Maftah, iwapo angepata nafasi ya kufanya hivyo.
Kocha huyo aliwaona wachezaji hao walipokuwa wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu yake, wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa. Simba ilifungwa mabao 3-0.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ouma alisema wachezaji hao wana viwango vya juu sana na angependa kuwaona siku moja wakichezea timu yake.
Alisema angepata nafasi katika timu yake, angewachukua kwa kuwa anaamini wangeisaidia, hususan katika michuano ya kitaifa na kimataifa kwa kuwa kwa jinsi alivyowaona uwezo wao unaruhusu.
“Nimevutiwa zaidi na Ngassa pamoja na yule beki aliyecheza namba tatu (Maftah), naamini kama ningewapata wale, kikosi changu kingekuwa imara sana kwa kuwa wanajituma uwanjani na pia wanaonyesha kutaka ushindi,” alisema Ouma.na hivyo wachezaji wa Tanzania wanaangaliwa kila nchi kwa hiyo ni faraja kwetu kuona wachezaji wanaaminiwa katika nchi za jirani.

0 comment.:

Post a Comment