kutoka kwa shafii daudiHatimaye leo hii sakata la uhamisho wa Mbuyu
Twite na Kelvin Yondani waliosajiliwa na klabu ya Yanga na kuwekewa pingamizi na
timu ya Simba limefikia mwisho baada ya wachezaji hao kuidhinishwa na kamati ya
sheria, maadili na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka TFF, chini
mwenyekiti mwanasheria Alex Mgongolwa, kuichezea klabu bingwa ya Afrika
mashariki na kati Dar Young Africans.
Kwa taarifa
za uhakika nilizozipata kutoka ndani ya shirikisho la soka nchini ni kwamba
wakati kamati ya maadili na sheria ilipokaa mkutano wa kujadili mapingamizi ya
wachezaji hao ilishindikana kabisa kwa wajumbe wa kamati kufikia makubaliano juu
ya hukumu ya mapingamizi hayo hasa la Kelvin Yondan na hapo ndipo ikamuuriwa
kwamba zipigwe kura miongoni mwa wajumbe kuamua ni wapi mchezaji huyo akacheze
msimu kati ya Yanga au Simba ambazo zote zina mkataba naye. Wajumbe wakapiga
kura na hatimaye kura nyingi zikachague aidhinishwe ajiunge na
Yanga.
Kwa upande wa suala la
mchezaji Mbuyu Twitte liliamuariwa kwa Yanga iwalipe Simba kiasi cha $32,000
ambazo Simba walimlipa Mbuyu Twitte ajiunge nayo kabla ya Yanga kuwazidi nguvu
mahasimu wao na kumtwaa mchezaji huyo huku akiwa tayari kashasaini mkataba na
Simba, malipo haya yafanyike ndani ya siku 21 na baada ya hapo Twitte atakuwa
huru kukipiga jangwani.
8:01 PM
0 comment.:
Post a Comment