DK 90: Simba 0 - 0 Mgambo
DK 84: Okwi anapiga shuti kali linalogonga mwamba na kurudi uwanjani.
DK: 80: Muda unazidi kuyoyoma na Simba wanaendelea kulishambulia lango la Mgambo. Pia wanaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji anatoka Ngasa anaingia Edo Christopher.
DK 70: Cholo anaingia vizuri mpaka kwenye sita ya Mgambo lakini anatoa krosi mbovu inayotoka nje.
DK 66: Issa Kinduru anapiga shuti kali katika lango la Simba na linatoka pembeni kidogo mwa goli.
DK 57: Simba wanaamka sasa, Amir Maftah anachezewa rafu nje kidogo ya eneo la hatari na Okwi anapiga faulo inayotoka nje kidogo ya lango la Mgambo.
DK 51: Simba 0 - 0 Mgambo
Kipindi cha pili kimeanza kati ya Simba na Mgambo JKT uwanja wa Mkwakwani.
HALF TIME
DK 43: Jonas Mkude anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Mgambo.
DK 38: Mgambo wanalisakama sana lango la Simba lakini ukosefu wa umakini ndani ya 18 unawagharimu magoli.
DK 35: Milango bado migumu timu zote zinashambulianakwa zamu lakini wanashindwa kutumia vizuri nafasi wanazopata.
DK 28: Mgambo wanaingia kwenye lango la Simba na kufanya shambulizi kali lakini shuti linalopigwa na mchezaji Issa Kinduru linadakwa na Juma Kaseja.
DK 25: Kwa muda sasa Mrisho Ngassa amekuwa akiisumbua sana ngome ya Mgambo, anafanya shambulizi kali kwa ku[piga shuti linatoka nje kidogo ya lango la Mgambo.
DK 20: Simba 0 - 0 Mgambo
DK 15: Timu ya JKT Mgambo inaonekana kucheza vizuri zaidi ya Mnyama, wakijituma kufanya kila wanachoweza kuweza kupata bao la mapema.
DK 5: Simba 0 - 0 Mgambo
Mpira umeanza hapa uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga.
VIKOSI VINAVYOANZA
SIMBA1: Juma Kaseja
2: Said Nassoro Chollo3: Amir Maftah4: Hassan Hatibu5: Pascal Ochieng6: Jonas Mkude7: Amri Kiemba8: Mwinyi Kazimoto9: Sunzu10: Okwi11: Mrisho Ngassa
MGAMBO1: Gudson Mmasa2: Yasin Awadhi3: Salu Mlima4: Bakary Msama5: Salum Kipana6: Ramadhan Malima7: Chande Magoja8: Musa Ngunda9: Issa Kanduru10: Fuly Maganga11: Juma Mwinyimvua
Home
»
»Unlabelled
»
Sunday, October 21, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment.:
Post a Comment