AZAM FC
imezunduka tena baada ya kuichapa JKT Oljoro 1-0 kwenye Uwanja wake wa Azam
Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara jioni hii.Shujaa wa
Azam leo alikuwa ni mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre Herman Tcheche aliyefunga
bao hilo pekee dakika ya nne kwa mkwaju wa penalti, baada ya Yassin Juma kuunawa
mpira kwenye eneo la hatari. Katika mchezo huo, Azam ilimpoteza kiungo wake
Himid Mao dakika ya 88 aliyelimwa kadi nyekundu kwa kucheza
rafu.Ushindi huo,
unaifanya Azam ifikishe pointi 24 baada ya kucheza mechi 12 na sasa inapanda
hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiizidi Simba kwa pointi moja,
ambayo pia imecheza mechi 12. Yanga yenye pointi 26, inaendelea kuongoza ligi
hiyo baada ya kucheza mechi 12 pia. Katika mechi
nyingine za ligi hiyo, bao pekee la Daniel Lyanga dakika ya tatu, limeipa
ushindi wa 1-0 Coastal Union dhidi ya Polisi Moro Uwanja wa Mkwakwani, Tanga,
wakati bao pekee la beki Issa Rashid dakika ya 26 limeipa Mtibwa Sugar ushindi
wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Manungu, Turiani
Morogoro.Ligi hiyo
inatarajiwa kuendelea Jumamosi, Simba na Toto African Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, Mgambo JKT na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, African Lyon na Mtibwa
Sugar Chamazi, Dar es Salaam, Prisons na JKT Ruvu Sokoine, Mbeya, Kagera Sugar
na Polisi Morogoro, Kaitaba, Bukoba na JKT Oljoro na Ruvu Shooting Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid, Arusha.Mchezo wa
kukamilisha mechi za mzunguko wa kwanza utachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
Jumapili kati ya Yanga na Coastal Union.
0 comment.:
Post a Comment