Kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen anatarajia kutangaza kikosi kitakachoshiriki michuano ya kombe la Chalenji siku ya ijumaa. Michuano ya Chalenji imepangwa kufanyika mjini Kampla Uganda kuanzia Disemba8 mpaka24. Poulsen alisema anataraji kuweka majina ya wachezaji hao siku ya ijumaa na kuingia kambini tayari kwa maandalizi ya mashindano hayo. Poulsen alisema katika uteuzi wa kikosi hicho atazingatia mambo makuu ikiwemo nidhamu,kujituma pamoja na umri ili kupata wachezaji watakaoweza kuiwakilisha vyema Tanzania na kufanikiwa kutwaa kombe hilo. “Nipo katika maandalizi ya mwisho na nafikirii siku ya ijumaa nitatangaza kikosi kitakachoingia kambini wiki ijayo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya Chalenji,nategema kambi inaweza kuwa hapa au Mwanza lakini mpaka nipate kauli ya mwisho ya viongozi wangu ambao ni TFF juu ya hatma ya kambi”alisema Poulsen. Michuano ya Chalenji itashiriki timu 11 za ukanda wa Afrika Mashariki na kati huku Zimbabwe na Zambia zikiomba kushiriki mwaka huu. Bingwa mtetezi wa michuano hii ni timu ya Taifa ya Uganda, ‘Uganda Cranes’ ambayo iliiondosha Taifa Stars katika hatua ya Fainali mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam
0 comment.:
Post a Comment