MARIO Balotelli sifa
yake kubwa ni utukutu na kadi kibao uwanjani- basi katika Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara ukiwasaka wachezaji wenye sifa kama za Mtaliano huyo mwenye asili
ya Ghana anayechezea Manchester City unaweza kuwapata kwa urahisi katika klabu
ya African Lyon ya Dar es Salaam.
Hadi sasa, ikiwa
imecheza mechi 11 za Ligi Kuu, Lyon inaongoza kwa adhabu za kadi, ikiwa ina kadi
30, kati hizo mbili ni nyekundu na 28 za njano.
Mtibwa Sugar inafuatia
kwa kuwa na watukutu wengi kikosini, hadi sasa ikiwa na kadi 22, kati ya hizo
mbili ni nyekundu.
Mgambo ndio inafuata
kwa kuwa na akina Balotelli wengi, hadi sasa ikiwa imepewa kadi 23, ingawa
bahati nzuri kwao zote ni za njano, wakati Toto African ni ya tatu kwa kucheza
mchezo usio wa kiungwana, ikiwa ina kadi 22, kati ya hizo moja nyekundu.
JKT Oljoro nayo pia ni
pango la watukutu, kwani hadi sasa ina kadi 21 na kati ya hizo mbili nyekundu,
Azam nayo si haba akina Balotelli wapo wapo, kwani hadi sasa katika mechi 10
ilizocheza imevuna kadi 16, moja nyekundu, sawa kabisa na Coastal Union na
Polisi Morogoro.
Prisons, Ruvu Shooting
na JKT Ruvu, zote zina kadi 16 za njano tupu kila mmoja, wakati kwa wapinzani wa
jadi, Yanga wanawazidi Simba kwa mchezo wa kiungwana, hadi sasa wana kadi 10 za
njano na moja nyekundu, wakati mahasimu wao wana kadi 13 za njano na mbili
nyekundu. Kagera Sugar wana kadi 14m, zote za
njano.
P Y R T
AFRICAN LYON 11
28 2 30
MGAMBO JKT 10
23 0 23
MTIBWA SUGAR 10
20 2 22
TOTO AFRICAN 11
21 1 22
JKT OLJORO FC 11
19 2 21
COASTAL UNION 11
14 2 16
POLISI
11 15 1 16
AZAM FC
10 15 1 16
PRISONS FC
9 16 0 16
RUVU SHOOTING 10
16 0 16
JKT RUVU SC
10 16 0 16
SIMBA SC
11 13 2 15
KAGERA SUGAR 11
14 0 14
YANGA SC
11 10 1 11
(P idadi ya mechi
ilizocheza, Y njano, R nyekundu na T ni jumla)
0 comment.:
Post a Comment