SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko ya mechi kadhaa za Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara baada ya kutokea dharura, hivyo kushindwa kufanyika kwa
mujibu wa kanuni.
Taarifa
kutoka TFF, zimesema kwamba sababu za mabadiliko hayo ni timu ya Tanzania
Prisons kupata ajali wakati ikienda Tanga kwa ajili ya mechi dhidi ya Mgambo
Shooting na mvua kubwa iliyonyesha mjini Mwanza na kusababisha kutofanyika kwa
mechi ya Oktoba 31 mwaka huu kati ya Toto Africans na Kagera
Sugar.
Sasa Mgambo
Shooting na Tanzania Prisons zitamenyana Novemba 14 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga,
Ruvu Shooting na Prisons Novemba 18, Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani,
Mtibwa Sugar na JKT Ruvu Novemba 7 Uwanja wa Manungu, Morogoro, Kagera Sugar na
Prisons Novemba 4 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na Ruvu Shooting na Toto Africans
siku hiyo Mabatini, Pwani.
Mabadiliko
hayo ya mechi za Ligi Kuu yameingilia hadi mechi za Ligi Daraja la Kwanza na
sasa Tessema na Ndanda waliokuwa wamenyane Novemba 4, Uwanja wa Mabatini,
watacheza Novemba 5 katika uwanja huo huo.
Mabadiliko
hayo yanaipisha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Toto
Africans ambayo itachezwa Novemba 4, kwenye uwanja huo
huo.
Ashanti
United na Tessema zilizokuwa zicheze Uwanja wa Mabatini Novemba 7, sasa
zitacheza siku inayofuata, Novemba. Mabadiliko hayo ni kutoa fursa ya kupumzika
kwa Tessema ambayo Novemba 5 itacheza na Ndanda
0 comment.:
Post a Comment