TIMU ya
taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imelalamikia Uwanja mbovu wa Chuo
Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, waliopelekwa kufanya mazoezi leo
kujiandaa na mechi ya kesho ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Tusker Challenge 2012 dhidi ya Sudan, itakayopigwa kwenye Uwanja wa
Mandela, Namboole mjini hapa.Ofisa Habari
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura amewasilisha malalamiko
hayo kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rodgers Mulindwa
ambaye ameahidi kuyafanyia kazi.“Tutalifanyia
kazi suala hilo, tutakuwa na kikao kesho litawasilishwa na litapatiwa usumbufu,
mwanzo huwa na matatizo, lakini mambo yatakuwa mazuri,”alisema
Mulindwa.Hata hivyo,
inashangaza Stars kupelekwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya
Biashara, wakati kwenye mpango wa awali kabisa wa FUFA ilitakiwa kufanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Nakawa. Kwa upande
wake, kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesikitishwa na
kutowasili kwa washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).“Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu
hawajafika, lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na
wachezaji waliopo,” alisema.“Nina imani
TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni
lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,”
alisema.Alisema
wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi
ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia
0 comment.:
Post a Comment