Home
»
»Unlabelled
»
Friday, November 23, 2012
UMOJA wa wanamichezo waliowahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara wenye maskani yao mjini Bukoba, Kagera, Bukoba Veteran Sports Club ni katika kuhamasisha ushiriki wa timu za Tanzania, Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes, kwenye michuano ya Kombe la Tusker Challenge inayofanyika jijini Kampala Uganda, umeandaa safari ya mashabiki walioko mkoani humo Kanda ya Ziwa kwa ujumla kwenda kushangilia mechi za timu hizo.Katibu Mkuu wa Bukoba Veterans, Shijja Richard ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba kwa kuanzia, mashabiki hao wataondoka mjini Bukoba Jumapili Novemba 25, 2012 kwenda kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Sudan Kaskazini.Amesema nia na madhumuni ya safari hiyo ni kuhamasisha wachezaji wa timu za taifa za Tanzania waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kutoa hamasa kwa watanzania kujenga tabia ya kushangilia timu zao na pia wanadhani kuwa ushiriki wao utaongeza ushindani katika michuano hiyo.Amesema tayari taratibu zote zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ili wawasiliane na mamlaka zinazohusika kwa ajili ya kupatiwa eneo maalumu uwanjani litakalowezesha watanzania waweze kuishangilia vizuri timu ya taifa.“Tunatarajia kwenda uwanjani na zaidi ya mashabiki 60 ambao hivi sasa wanakamilisha taratibu za mwisho za kuvuka mpaka wa nchi. Matarajio yetu ni kuendelea kuziunga mkono timu za taifa katika michuano hiyo hadi kufikia mwisho wa michuano. Tunaomba watanzania wengine walioko kanda ya ziwa katika mikoa ya Shinyanga, Mara na Mwanza watuunge mkono,”alisema Richard.Kikosi cha kinatarajiwa kuwasili leo mjini Kampala, kikitokea Mwanza tayari kwa mashindano hayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Tusker Challenge 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho.Stars imekuwa kambini mjini Mwanza kwa takriban wiki mbili sasa ikijifua vikali chini ya kocha wake, Mdenmark Kim Poulsen kujiandaa kwenda kutwaa taji la nne la Challenge.Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichopo kambini mjini Mwanza, kinaundwa na makipa; Juma Kaseja (Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’ wa Azam FC, mabeki; Kevin Yondan (Yanga), Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment.:
Post a Comment