Friday, July 12, 2013

11:24 AM
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema kwamba ameiandaa vyema timu yake kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Uganda, The Cranes kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao pekee.
Mei 26, 2012

REKODI YA KIM POULSEN STARS

Tanzania 0 – 0 Malawi (Kirafiki)
Juni 2, 2012
Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 10, 2012
Tanzania 2 – 1 Gambia (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 17, 2012
Msumbiji 1 – 1 Tanzania  (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
Agosti 15, 2012
Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
Novemba 14, 2012
Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)
Desemba 22, 2012
Tanzania 1-0 Zambia (Kirafiki)
Januari 11, 2013
Tanzania 1-2 Ethiopia (Kirafiki)
Februari 6, 2013
Tanzania 1-0 Cameroon (Kirafiki)
Machi 24, 2013
Tanzania 3-1 Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 2, 2013
Sudan 0 – 0 Tanzania (Mechi ya kirafiki Ethiopia)
Juni 8, 2013 
Morocco 2-1 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 16, 2013
Tanzania 2-4 Ivory Coast (Kufuzu Kombe la Dunia)

Kim ameyasema hayo leo asubuhi katika Mkutano wa pamoja na mpinzani wake, Mserbia Milutin Sredojvic ‘Micho’ wa The Cranes na Waandishi wa Habari kuhusu mchezo huo wa kesho uliofanyika katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam.
Tanzania na Uganda zipo katika kambi jirani, Kariakoo, Dar es Salaam, Stars wakiwa hoteli ya Tansoma na Cranes hoteli ya Sapphire Court, maeneo ya Gerezani. 
Makocha wote waliezea ubora wa wapinzani, lakini wakasisitiza kuwa wanaingia uwanjani kuhakikisha wanashinda ili kujiweka katika mazingira mazuri kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa Kampala wiki mbili zijazo.
Kim alisema Uganda ndiyo inayoongoza kwa ubora wa viwango vya FIFA katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, hivyo ni changamoto kwao ingawa wachezaji wake tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.
Naye Micho aliyefuatana na nahodha wake, Hassan Wasswa alisema Taifa Stars imekuwa ikifanya vizuri tangu iwe chini ya Kim, na itakuwa na wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kinachocheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia wakati kwa upande wake atakuwa na wachezaji wawili tu.
Mchezo wa kesho utakuwa wa 13 kwa Kim tangu aanze kuinoa Stars, akirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen baada ya kupandishwa kutoka timu za vijana. 
Katika michezo hiyo 13, Kim ameiwezesha Stars kushinda mechi tano, sare nne na kufungwa nne, ikifunga jumla ya mabao 16 na kufungwa 16 katika mechi zote hizo, kipigo kikubwa zaidi kikiwa 4-2 nyumbani mwezi uliopita kutoka Ivory Coast na ushindi mnono ukiwa wa 3-1 kutoka Morocco Machi mwaka huu.

0 comment.:

Post a Comment