SIMBA SC tayari ipo wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ambako itacheza mchezo mmoja wa kujipima nguvu na Kahama United Jumapili kwenye wa Manispaa wilayani humo.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ amesema kwamba baada ya mchezo huo wa Jumapili, timu itaelekea Musoma mkoani Mara kucheza mechi moja zaidi.
Amesema mjini Musoma watacheza na kombaini ya Musoma kwenye Uwanja wa Karume Jumatano, yaani Julai 17 na baada ya hapo timu itarejea Dar es Salaam.
URA ya Uganda inatarajiwa kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza na Simba SC Julai 20, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Simba, kabla ya kwenda Kahama ilikwenda Katavi ambako ilicheza mechi mbili na kushinda zote, 3-1 dhidi ya Rhino FC ya Tabora na 2-1 dhidi ya kombaini ya Katavi kwenye Uwanja wa wazi wa Katavi mkoani humo.
Simba SC, ambayo ilikuwa Katavi kwa mwaliko wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mchezo wake wa kwanza, mabao yake yalifungwa na Edward Christopher mawili na moja Nahodha mpya, Nassor Masoud ‘Chollo’ na mchezo uliofuata mabao yalifungwa na Kun James mshambuliaji aliye katika majaribio kutoka Al Ahly Shandi ya Sudan Kusini na beki Mganda, Samuel Ssenkoom aliyesajiliwa kutoka URA.
Home
»
»Unlabelled
» SIMBA SC tayari ipo wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ambako itacheza mchezo mmoja wa kujipima nguvu na Kahama United Jumapili kwenye wa Manispaa wilayani humo.
Friday, July 12, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment.:
Post a Comment