Thursday, February 13, 2014

2:16 PM

AZAM FC imefika salama mjini Beira, Msumbiji tayari kwa mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Ferroviario de Beira Jumapili mjini humo.Msafara wa Azam ulioondoka bila kocha wake Msaidizi, Kalimangonga Sam Daniel Ongala ‘Kali Ongala’ ulifika jana na leo umeanza mazoezi kwenye Uwanja wa wenyeji wao hao.Mfungaji wa bao pekee la Azam Chamazi dhidi ya Feroviario, Kipre Herman Tchetche akiwa amejibanza kukwepa mvua inayoendelea mjini BeiraKatibu wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kutoka Beira kwamba timu imefikia katika hoteli ya Rainbow na mechi itachezwa Jumapili Saa 8:00 mchana kwa saa za Msumbiji na saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.Father amesema mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam TV. “Lakini mvua kubwa inanyesha huku, inanyesha kutwa nzima, ila maandalizi ni mazuri na tumekuja na viatu vya kuchezea kwenye mvua, hivyo tupo kamili,”alisema Father.Azam FC iliyoanza kwa ushindi mwembamba wa 1-0 Jumapili Uwanja wa Azam Complex Jumapili, iliondoka jana asubuhi Dar es Salaam kwa ndege ya Fast Jet hadi Johannesburg, Afrika Kusini ambako waliunganisha ndege ya shirika la Msumbiji kwenda Beira.Uwanja wa FerroviarioMvua kutwa nzimaWachezaji wakiwa uwanjani tayari kwa mazoeziAzam imeondoka na wachezaji 21 ambao ni makipa; Mwadini Ali, Aishi Manula na Jackson Wandwi, mabeki Luckson Kakolaki, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Aggrey Morris, Said Mourad, David Mwantika, viungo Ibrahim Mwaipopo, Kipre Balou, Jabir Aziz, Salum Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha na washambuliaji John Bocco, Kipre Tchetche, Brian Umony, Seif Abdallah, Gaudence Mwaikimba na Ismael Kone.Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Mcameroon, Joseph Marius Omog, kocha wa makipa Iddi Abubakar, Meneja Jemadari Said, Daktari Mkuu Mwanandi Mwankemwa, Mchua misuli Paul Gomez na mtunza vifaa Yussuf Nzawila. Azam inahitaji sare yoyote baada ya ushindi wa 1-0 nyumbani ili kusonga mbele.


Posted via Blogaway

0 comment.:

Post a Comment