Wednesday, August 15, 2012

3:02 PM
kikosi cha simba sport club B..
kikosi cha Azam football club..
full shangwe
bao la kwanza kwa Simba sport club.
fullshangweeeeeee..
hatari langoni mwa Azam..
goalllllll goallllllllllllll bao la pili simba sport club.........

SIMBA SC imetinga Fainali ya michuano ya BankABC Sup8R baada ya kuifunga Azam FC, mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Jumamosi itamenyana na Mtibwa Sugar, ambayo katika mechi ya kwanza imeifunga Jamhuri ya Pemba mabao 5-1, uwanja huo huo.
Hadi mapumziko, Simba inayotumia wachezaji wake wa kikosi cha pili, Simba B, kinachofundishwa na Suleiman Matola, walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na Rashid Ismail aliyeunganisha krosi ya Edward Christopher dakika ya pili tu ya mchezo huo.
Kipindi cha pili ‘Watoto wa Matola’ walirudi na moto na kulisakama kama nyuki lango la Azam, wakigongeana pasi za uhakika ndefu na fupi na kuwafunika kabisa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi.
Christopher Edward aliifungia Simba bao la pili kwa penalti dakika ya 56, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa ndani ya eneo la hatari na Luckson Kakolaki.
Azam walipata bao la kufutia machozi dakika ya 71, mfungaji Zahor Pazi aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Gaudence Mwaikimba, baada ya kutokea purukushani kwenye lango la Simba B.
Ushindi huu wa Simba B ni sawa na kuwalipia kisasi kaka zao, Simba A ambao walifungwa na Azam 3-0 katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame mwezi uliopita.
Katika mchezo huo, kikosi cha Smba kilikuwa; Abuu Hashimu(18), Miraj Adam (19), Omary Salum (11)/William Lucian ‘Gallas’, Hassan Isihaka (5), Hassan Hatibu (15) Said Ndemla (13), Haroun Athumani (7), Abdallah Seseme (17), Rashid Ismail (8), Edward Christopher (9)/Ramadhan Mzee na Frank Sekule (4)Ibrahim Ajibu.
Benchi; Saleh Malande (1), Ramadhan Mzee (2), William Lucian ‘Gallas’(3), Kenny Alex (12), Mohamed Salum (16), Ibrahim Ajibu (20) na Jesse Nyambo (14). 
Kocha; Suleiman Matola. Msaidizi; Amri Said.

0 comment.:

Post a Comment