Kwa mujibu
wa tovuti ya Azam Fc Mchezaji John Bocco amerejea kwenye kikosi cha Azam FC baada
ya majaribio ya
wiki mbili.
Maribio
hayo yaliishia kwa kukubalika na
kocha mkuu wa Super
Sport United Gavin Hunt lakini
bahati mbaya uongozi wa
SUFC ulishindwa kutoa ofa
ya kueleweka kwa
John Bocco na Azam
FC.
SuperSport United FC ilimtaka Bocco kwa
mkopo huku wakisema kuwa kwa
sasa hana uwezo wa
kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu yao.
Lakini pia
SUFC ilishindwa kuweka wazi maslahi ya
mchezaji. Maelezo ya
Uongozi wa SuperSport United FC ilikuwa ni
kumuomba Bocco kwa
mkopo kwa kuwa
wanahitaji kumuona kwanza akifunga kwenye ligi
ya Afrika ya
Kusini kabla hawajafikiria ofa ya kumnunua.
Wakala
wa mchezaji John Bocco Bw.
Yusuf Bakhresa aliwataka Supersport United kumuonesha mkataba ambao wataingia na
John Bocco na kueleza maslahi ambayo watakuwa wakimlipa lakini ilishindikana zaidi ya
kusisitiza kuwa wanahitaji muda kabla hawajaingia mkataba mzuri na
Bocco.
Yusuf
hakufurahishwa na kitendo hicho na
aliwataka SUFC kuwa
wawazi kama wanamtaka John Bocco na
watoe ofa itakayoizidi Azam FC vinginevyo itakuwa vigumu kumpata.
Azam FC
imeamua kubaki na
nyota wake huyu mwenye umri wa
miaka 23 lakini milango ipo
wazi kwa SuperSport kuendelea kumfuatilia na itakapotokea kuwa wamejiridhisha na kiwango chake basi
walete ofa yao.
John
Bocco binafsi baada ya
kurejea nchini alisema amefurahishwa na mazingira ya
Supersport United lakini akaomba kuwa angependa kupata maslahi makubwa zaidi ya
Azam FC vinginevyo haoni sababu ya
kwenda Afrika ya
Kusini bila maslahi mazuri kwani Azam
FC sasa ni timu
kubwa Afrika Mashariki na
mwakani itashiriki mashindano ya shirikisho barani Afrika.
10:44 AM
0 comment.:
Post a Comment