MCHEZO wa raundi ya kwanza ya ligi kuu soka Tanzania Bara baina ya watani wa jadi nchini, Simba na Yanga utarushwa ‘Live’ kupitia kituo cha televisheni cha Super Sport chenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.
Mechi hiyo ambayo itachezwa Oktoba 3 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa mechi tano za ligi hiyo zitakazorushwa ‘live’ na kituo hicho kwa mwaka huu.
kikosi cha simba sport club.-tanzania |
kikosi cha yanga-tanzania. |
hawa watu wa super sport wandishi wa habari. |
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa habari wa Shiriukisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema kwamba hatua hiyo imetokana na kuwepo kwa mazungumzo ya udhamini wa kituo hicho kwa ligi kuu utakaoanza mwakani.
Alisema kutokana na mazungumzo hayo kutokamilika wameona waanze kwa majaribio kwa kuonesha mechi hizo tano na mwakani wataendelea na ratiba nyingine baada ya mipango kukamilika.
“Kama mjuavyo Super Sport wana ratiba zao na mambo mengi hivyo inabidi kujipanga kwanza, lakini mazungumzo yanakwenda vizuri na ndiyo maana kwa kuanzia wataonesha mechi hizo tano.
Mbali na mechi hizo, Wambura alisitaja mechi nyingine zitakazorushwa ‘Live’ na kituo hicho ni pamoja na ule wa Azam Fc dhidi ya JKT Ruvu utakaochezwa Uwanja wa Chamazi, pamoja na ule wa Simba na Prisons utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salam ambapo mechi hizo zote zitafanyika Septemba 28.
Mchezo mwingine ni kati ya Yanga dhidi ta African Lyon utakaochezwa Septemba 30 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, sambamba na ule wa Ruvu Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa katika dimba la Chamazi.
Ligi kuu soka Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 15 mwaka huu chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
0 comment.:
Post a Comment