Saturday, September 15, 2012

1:27 PM

NA fzakar.blog
Kikosi cha simba sport club:
Kikosi cha Afican lyon
Emmanuel Okwi akiwatoka hapa wachezaji wa African lyon:
Akuffor akishangilia goli lake la kwanza:
Emmanuel okwi akishangilia goli lake la Pili:
Mrisho khalfan ngasa akifunga goli lake la Tatu:
Nassor Masoud 'Chollo' anatia krosi
chollo anamtupia krosi nassoro massoud:
SIMBA SC imeanza vema kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jioni hii baada ya kuichapa mabao 3-0 African Lyon katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Emanuel Okwi dakika ya 33 baada ya kuwatoka mabeki wa Lyon na Nassor Masoud ‘Chollo’ dakika ya 36 akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa.

Lyon walikosa penalti dakika ya 35, baada ya mkwaju wa Sunday Bakari kupanguliwa na Juma Kaseja, kufuatia Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Kipindi cha pili, Lyon kidogo walirekebisha makosa yao, lakini bado Simba iliendelea kutawala mchezo na dakika ya 56, Danniel Akuffor aliifungia timu yake bao la kuhitimisha ushindi kwa mkwaju wa penalti, baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Lilikuwa ni goli ya tano kwa Akuffor katika mechi sita tangu alipojiunga na Wekundu wa Msimbazi akitokea Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Alifunga goli moja wakati Simba walipoibwaga JKT Oljoro 2-1, akafunga pia moja katika ushindi 2-1 dhidi ya Mathare United na jingine moja katika sare ya 1-1 dhidi ya Sony Sugar ya Kenya katika mechi tatu za kirafiki zilizopigwa mjini Arusha.

Katika mechi ya nne ya kirafiki ambayo Simba  walilala 3-0 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, Akuffor alizimia uwanjani na kutolewa katika dakika ya 40 akiwa hajafunga, lakini alirejea kucheka na nyavu dhidi ya Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii ambayo Simba walishinda 3-2, yeye akifunga moja kwa njia ya penalti kabla ya leo kukamilisha bao lake la tano katika mechi sita.

Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo/Ramadhan Chombo, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma na Emanuel Okwi.

African Lyon; Abdul Seif, Johanes Kajuna, Hamadi Manzi, Sunday Bakari, Benedictor Mwamlangala, Sunday Hinju, Obina Salamusasa, Semmy Kessy, Iddi Mbaga, Jacob massawe na Yussuf Mlipili.

Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Hamisi Kiiza, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Nizar Khalfan/Athumani Iddi, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Didier Kavumbangu/Simon Msuva na Stefano Mwasyika.

Kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, bao pekee la Abdulhalim Humud liliipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.

Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Ibrahim Mwaipopo,  Himid Mao/Jabir Aziz, John Bocco, Abdi Kassim/Kipre Balou na Kipre Herman Tchetche.

Kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, bao pekee la kiungo Mkenya, Jerry Santo dakika ya 41 liliipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Mgambo FC.

Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji Polisi wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu.

Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans imelazimishwa sare ya 1-1 na JKT Oljoro, wakati Uwanja wa Chamazi, Mbagala, JKT Ruvu imeifunga Ruvu Shooting mabao 2-1.

MATOKEO MECHI ZOTE LIGI KUU LEO
Simba 3-0 African Lyon
Kagera Sugar 0-1 Azam FC
Prisons 0-0 Yanga
Coastal Union 1-0 Mgambo JKT
Toto African 1-1 JKT Oljoro
Polisi Moro 0-0 Mtibwa Sugar
JKT Ruvu 2-1 Ruvu Shooting 

0 comment.:

Post a Comment