Tuesday, November 13, 2012

4:29 PM

MDHAMINI wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kilimanjaro Premium Lager amewataka wachezaji wa timu hiyo kuonyesha nidhamu ya hali ya juu wakiwa kambini Mwanza na pia kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi zijazo hususani katika mechi ya Jumatano ya kirafiki dhidi ya Harambee Stars.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, amesema wao kama wadhamini wana imani na timu ya taifa na Kocha wake Kim Poulsen.“Mechi zilizochezwa mpaka sasa hivi tangu tumechukua udhamini zinaridhisha kwa kuwa tumeona kiwango cha timu kikikua siku hadi siku..tuna imani mechi ya Jumatano dhidi ya Harambee Stars tutashinda,” slisema Bwana Kavishe.Alisema moja ya vitu ambavyo wachezaji wanatakiwa kuzingatia sana ni nidhamu nje na ndani ya uwanja kwani mpira ndio ajira yao kwa hivyo lazima waitetee na kuilinda vizuri.“Kocha wa sasa hivi anazingatia sana nidhamu na hili lina umuhimu sana katika soka hata uwende wapi duniani..unaweza kuwa mchezaji mzuri sana lakini bila nidhamu kocha anaweza kukuacha katika kikosi chake na kuwachezesha wachezaji wenye nidhamu,” alisema.Bwana Kavishe aliendelea kusema kuwa wamefurahishwa na kitendo cha TFF kuipeleka timu Mwanza kucheza mechi ya kirafikii dhidi ya Kenya na pia kujiandaa na mashindano ya CECAFA Challenge yanayotarajia kuanza Jijini kampala tarehe 24 mwezi huu.“Hali ya hewa ya Mwanza na ya Kampala hazipishani sana kwa hivyo tunaamini huu ulikuwa uamuzi sahihi kabisa ili wachezaji wazoee hali ya hewa, alisema.Stars inashuka dimbani Jumatano saa kumi alasiri dhidi ya Harambee Stars ya Kenya katika Uwanja wa Kirumba. Tangu Stars ipate mdhamini mpya, Kilimanjaro Premium Lager, imeshacheza dhidi ya Ivory Coast, Msumbiji, Botswana na Namibia .Kilimanjaro Premium Lager imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni mbili kuidhamini Taifa Stars kwa miaka mitano ijayo.

0 comment.:

Post a Comment