Sunday, December 9, 2012

9:23 AM

AJABU na kweli. Robert Ssentongo amepewa tuzo ya ufungaji wa Kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge jana, wakati anazidiwa mabao na washambuliaji wa Tanzania Bara, John Raphael Bocco na Mrisho Khalfan Ngassa, ambao kila mmoja ana mabao matano.
Ssentongo amemaliza mabao manne, lakini jana CECAFA ikampa tuzo hiyo na kuwaacha wengi midomo wazi.
Uganda ilitwaa Kombe la Chalenge jana kwa kuifunga Kenya mabao 2-1, ambayo yote Kenya walijfunga jana kupitia kwa wachezaj wao Anthony Kimani na Joackins Atudo. Bao la Kenya lilifungwa na Edwin Lavatsa.
Mbali na Ngassa na Bocco kuongoza wakifuatiwa na Ssentongo, wengine waliokuwamo kwenye kinyang’anyiro ni Brian Umony wa Uganda aliyemaliza na mabao matatu, sawa Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar, Suleiman Ndikumana na Chris Nduwarugira wa Burundi.
Wachezaji wenye mabao mawili kila mmoja ni Geoffrey Kizito wa Uganda, David Ochieng, Mike Barasa, Clifton Miheso wa Kenya na Dadi Birori wa Rwanda.

WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
John Bocco Tanzania 5
Mrisho Ngassa Tanzania 5
Robert Ssentongo Uganda 4
Brian Umony Uganda 3
Khamis Mcha Zanzibar 3
Suleiman Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Chris Nduwarugira Burundi 3
Geoffrey Kizito Uganda 2
David Ochieng Kenya 2
Clifton Miheso Kenya 2
Dadi Birori Rwanda 2
Mike Barasa Kenya 2

0 comment.:

Post a Comment