Kikosi kizima cha timu ya Yanga ya jijiji Dar es
Salaam, kimeondoka leo jijini kuelekea nchini Rwanda ambako kitaweka kambi kwa
ajili ya mazoezi yake ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara, inayotarajia
kuanza mwezi ujao.
Mbali kambi hiyo pia kikosi hicho kimepata
mwaliko wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambapo kikosi hicho kikiongozana na
viongozi wake kitatinga Ikulu ya nchini humo kwa ajili ya kutambulisha Kombe lao
la ushindi wa michuano ya Kombe la Kagame, iliyomalizika mwezi uliopita.
Kikiwa nchini humo kikosi hicho kinatarajia
kucheza michezo mitatu ya kirafiki ambapo mchezo wa kwanza utakuwa ni kati yao
na timu ya Royal Sports, mchezo wa pili utakuwa na Polisi na wa tatu utapangwa
baada y mchezo wao wa kwanza.
0 comment.:
Post a Comment