Mbwana Ally Samatta anazidi kung'ara kwenye soka
la anga ya kimataifa akiwa na klabu yake ya TP Mazembe.
Mbwana Samatta
ambaye tayari anatimiza mwaka mmoja tangu ajiunge na timu yake hiyo ya Kinshasa
Congo akitokea klabu bingwa ya Tanzania bara Simba Sports Club, amekuwa mmoja ya
wafungaji bora na tegemeo kabisa kwenye timu hiyo inayomilikiwa na tajiri Moise
Katumbi.
Kwa takwimu zilizo sahihi kabisa za Mbwana Samatta katika msimu
huu 2011/12 upande wa Ligi ya mabingwa wa Afrika amecheza mechi 7
tu.
Katika mechi hizo saba Samatta "Golden Boy" amefunga mabao 5. Katika
magoli hayo matano, kichwa chake kimeweka kambani mabao 4 na moja amefunga kwa
guu lake la kulia.
Mabao hayo matano ya Samatta kwenye Africa Champions
league amezifunga timu za Power Dynamo akiwa Ugenini, Akafunga bao lingine dhidi
ya Al Merreikh aTP wakiwa nyumbani kabla ya kuja kuwafunga tena Wasudan hao
nyumbani kwao Khartoum. Alhly wakawa majeruhi wengine wa Mbwana Samatta baada ya
kuwaumiza wakiwa kwao Misri. TP Mazembe wakiwa uwanja wao nyumbani Tanzania
Golden Boy akatupia bao moja kwenye mechi dhidi ya Berekum Chelsea. Ikafika zamu
ya waarabu Zamalek ambaye akawafunga bao moja moja nyumbani na Ugenini na
kutimiza mabao matano.
Dakika ambazo Mbwana Samatta anafunga sana magoli
ni kuanzia kati ya dakika ya 16-30 ambapo hapo amefunga mabao mawili. kuanzia dk
ya 31 mpaka 42 amafunga goli moja tu, huku akionekana kuwa hatari zaidi kwenye
dakika ya 75 ya mchezo kwani tayari ameshafunga mabao mawili kwenye dakika
hiyo.
Mafanikio hayo ya Samatta kwenye michuano mbalimbali TP
Mazembe inayoshiriki yamezidi kumuongezea thamani kwenye soko la usajili
duniani, kutoka kuuzwa kwa dola 100,000 na Simba kwenda TP Mazembe mpaka sasa
anakadiriwa kuwa na thamani ya £175,000 ambayo ni mara 3 ya zaidi TP waliilipa
Simba kumsaini Samatta.
6:59 PM
0 comment.:
Post a Comment